斯瓦希里语诗歌
作者:夏班·罗伯特(Shaaban·Robert)
译者:冯玉培
朗读:2018级斯瓦希里语 宋艺婷
Mapenzi Bora
Mapenzi ni jambo moja katika mambo yaliyo
muhimu na wajibu kwa mtu katika maisha yake.
Atakupenda nani katika dunia kama hutayari
kupenda wengine wala kuheshimu mapenzi yao?
Dunia tunayokaa,
Jangwa tupu la ukiwa,
Na kiu na njaa mbaya,
Na mateso na machozi.
Dunia jangwa la kiu,
Na sisi tusisahau,
Mapenzi faraja kuu,
Ya kuzima kiu hizi.
Mapenzi yana mwangaza,
Ni taa katika giza,
Na kitu cha kutukuza,
Kila palipo wakazi.
Mapenzi nitayasifu,
Mpaka siku ya ufu,
Maana ndiyo turufu,
Kwangu iliyo azizi.
仁爱为贵
仁爱乃重要之事,是人生之职责,
倘若你不爱他人也不尊重他人的爱,
那么,人世间又有谁会来爱你呢?
我们居住的地球,
纯属孤独的沙漠,
处处是干渴与饥饿,
磨难与眼泪。
世界乃干渴的沙漠,
我们不要忘记,
仁爱乃莫大的慰籍,
可以用它来止渴。
仁爱放射着光芒,
是黑夜里的一盏明灯,
凡是有人的地方,
理应予以推崇。
我要赞美仁爱,
直至生命终结,
此乃制胜王牌,
对吾弥足珍贵。
用户评论